Inafaa kwa mwoshaji kuelezea yale anayoyaona kwa maiti?

Swali: Baadhi ya wale wanaowaosha maiti huelezea yanayowakuta pindi wako wanawaosha maiti. Unasemaje?

Jibu: Kinachotakiwa kwa mwoshaji ni yeye kuficha yale aliyoyaona ikiwa si mazuri. Hata hivyo wanachuoni wamesema ikiwa maiti yule ni mtu wa Bid´ah ambaye analingania katika Bid´ah zake na mwoshaji akaona usoni mwake kuwa ni mwenye kuchukia bora ni kuyataja ili awatahadharishe watu [kutokamana na Bid´ah].

Upande mwingine ikiwa maiti ni mtu mwema na mwoshaji akaona mema ni bora kuyaeleza. Hilo ndani yake mna kujenga dhana nzuri na kumuombea du´aa yule maiti.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/91-90 )
  • Imechapishwa: 06/09/2021