Swali: Je, kipomoko kinaswaliwa, kuoshwa na kuvikwa sanda?
Jibu: Hakiswaliwi isipokuwa ikiwa kama kimeshapuliziwa roho, jambo ambalo linakuwa baada ya miezi mine. Hivo ndivo inavyofahamisha Hadiyth ya Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Hakika umbile la mmoja wenu linakusanywa tumboni mwa mama yake kwa siku arubaini. Kisha linakuwa pande la damu kwa muda kama huo. Kisha inakuwa kinofu cha nyama kwa muda kama huo. Halafu anatumiwa Malaika ambaye anayeamrishwa kuandika mambo mane; riziki yake, muda wake wa kueshi, matendo yake na kama atakuwa ni mla khasara au mwenye furaha.”[1]
Ikiwa kipomo kimeshafikisha miezi mine kinaswaliwa baada ya kuoshwa na kuvikwa sanda. Baada ya hapo kinazikwa pamoja na waislamu wenzake. Na ikiwa hakijafikisha miezi mine hakioshwi, hakivikwi sanda na wala hakiswaliwi. Kinaweza kuzikwa/kufukiwa sehemu yoyote katika ardhi.
[1] l-Bukhaariy (3028) na Muslim (01) na (2643).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/89-90)
- Imechapishwa: 06/09/2021
Swali: Je, kipomoko kinaswaliwa, kuoshwa na kuvikwa sanda?
Jibu: Hakiswaliwi isipokuwa ikiwa kama kimeshapuliziwa roho, jambo ambalo linakuwa baada ya miezi mine. Hivo ndivo inavyofahamisha Hadiyth ya Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Hakika umbile la mmoja wenu linakusanywa tumboni mwa mama yake kwa siku arubaini. Kisha linakuwa pande la damu kwa muda kama huo. Kisha inakuwa kinofu cha nyama kwa muda kama huo. Halafu anatumiwa Malaika ambaye anayeamrishwa kuandika mambo mane; riziki yake, muda wake wa kueshi, matendo yake na kama atakuwa ni mla khasara au mwenye furaha.”[1]
Ikiwa kipomo kimeshafikisha miezi mine kinaswaliwa baada ya kuoshwa na kuvikwa sanda. Baada ya hapo kinazikwa pamoja na waislamu wenzake. Na ikiwa hakijafikisha miezi mine hakioshwi, hakivikwi sanda na wala hakiswaliwi. Kinaweza kuzikwa/kufukiwa sehemu yoyote katika ardhi.
[1] l-Bukhaariy (3028) na Muslim (01) na (2643).
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/89-90)
Imechapishwa: 06/09/2021
https://firqatunnajia.com/kipomoko-kinaoshwa-kuvikwa-sanda-na-kuswaliwa/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)