Inajuzu kung´oa meno ya dhahabu ya maiti?

Swali: Ikiwa maiti yuko na meno ya dhahabu yatolewe?

Jibu: Ikiwa kuna uwezekano wa kuyatoa meno ya maiti bila ya usumbufu yatolewe. Kuyabakiza ni kuharibu pesa, jambo ambalo limekatazwa. Ikiwa hawezi kutolewa nayo mpaka kwa usumbufu yaachwe mpaka pale maiti atapooza kisha yachukuliwe.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/88)
  • Imechapishwa: 06/09/2021