Ni ipi hukumu ya kukata kucha za maiti, masharubu na nywele za sehemu ya siri?

Swali: Ni ipi hukumu ya kukata makucha ya maiti, kumkata masharubu, kunyofoa nywele za chini ya kwapa na kunyoa nywele za sehemu ya siri?

Jibu: Wanachuoni wamesema kumkata makucha maiti, kumkata nywele zinazohitajia kukatwa, kama nywele za sehemu ya siri, chini ya kwapa na masharubu, ni vizuri kukihitajia kufanya hivo. Kusipohitajia kufanya hivo zinaachwa na hazikatwi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/87-88)
  • Imechapishwa: 06/09/2021