Inafaa kumvua maiti nguo zote na akaonekana na wale wasiohitajika?

Swali: Baadhi ya wale wanaomuosha maiti wanamvua nguo zake zote na anabaki uchi na huenda kukaingia watu wasiokuwa na haja. Unaonaje juu ya hali hii?

Jibu: Wakati wa kumvua nguo maiti ni lazima kuwepo nguo inayofichika uchi wake. Wamesema kuwa inachukizwa wale wasiohitajika kuhudhuria uoshwaji wake. Kuhusu wale wanaohitajika – kama kukihitajika maji au mengineyo – ni sawa wakahudhuria.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/87)
  • Imechapishwa: 06/09/2021