Swali: Kipi kinachofanywa ikiwa haiwezekani kumuosha maiti?

Jibu: Ikiwa haiwezekani kumuosha maiti, wanachuoni wanasema kuwa inatakiwa kumfanyisha Tayammum. Ina maana ya kwamba mwoshaji anatakiwa kupiga mikono yake kwenye udongo halafu apanguse uso wa maiti na vitanga vyake vya mikono. Baada ya hapo avishwe sanda, aswaliwe na kuzikwa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/90 )
  • Imechapishwa: 06/09/2021