Swali: Je, inajuzu kwa mwanamke kusoma kwa sauti ya juu katika swalah ya Subh, Maghrib na ´Ishaa kama mwanaume au yeye anatakiwa kusoma kwa sauti ya siri?
Jibu: Ikiwa yuko peke yake nyumbani, yuko na Mahram zake au yuko pamoja na wanawake wenzake tu anaweza kusoma kwa sauti ya juu. Akiwaongoza wanawake wenzake katika swalah nyumbani kwake na wako wao wenyewe tu anaweza pia kusoma kwa sauti ya juu.
Ama ikiwa anaswali na pembezoni mwake kuna wanaume ambao ni ajinabi kwake wanasikia sauti yake, bora zaidi asisome kwa sauti ya juu.
- Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (126/04)
- Imechapishwa: 22/08/2020
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket
Related
Mwanamke anasoma kwa sauti ya juu kama mwanamme
Swali: Je, swalah ya mwanamme haitofautiani na ya mwanamke inapokuja katika kusoma kwa sauti ya juu na ulazima wa kukimu? Jibu: Adhaana na Iqaamah ni jambo maalum kwa wanamme. Hivo ndivo zilivyopokelewa dalili. Wanawake hawana adhaana wala Iqaamah. Kuhusu kusoma kwa sauti ya juu imesuniwa kwake kusoma kwa sauti ya…
In "Swalah ya mwanamke"
Swalah ya mkusanyiko ya wanawake masomoni
Swali: Ni ipi hukumu ya swalah ya mkusanyiko kwa mwanamke shuleni? Jibu: Swalah ya mkusanyiko kwa mwanamke sio lazima. Lakini hapana vibaya wakiswali pamoja ili baadhi wajifunze kutoka kwa wengine na wafaidishane. Imepokelewa kutoka kwa Umm Salamah na ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ya kwamba waliwaswalisha baadhi ya wanawake. Ni jambo…
In "Hukumu ya swalah ya mkusanyiko"
Tarawiyh mkusanyiko wanawake nyumbani II
Swali: Nataka kujua namna mwanamke anavoswali swalah ya Tarawiyh kama anaswali peke yake? Je, wanawake wanaweza kuswali mkusanyiko katika nyumba zao? Jibu: Ndio. Tarawiyh anatakiwa kutoa salamu kila baada ya salamu mbili. Mwanamke mwenziwe anaweza kuwaswalisha na atasimama katikati ya safu yao na asisimame mbele yao. Alete Takbiyr na anyanyue…
In "Tarawiyh kwa mwanamke"