Swali: Hadiyth inayosema fasiki hana usengenyi.

Jibu: Sitambui msingi wake. Hata hivyo ni yenye kuchukuliwa kutoka katika Hadiyth ambazo ni Swahiyh. Alipojiwa na bwana mmoja akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mwache aingie. Ndugu mbaya aliyoje!”[1]

Ikafahamisha kuwa hapana ubaya kumsengenya ambaye anadhihirisha uovu. Hadiyth iliyotangulia punde mmekwishaisikia ambapo lilipitishwa jeneza la mtu ambapo Maswahabah wakamsema vibaya akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Imewajibika.”[2]

Kwa hivyo mtu akidhihirisha shari na akafanya maasi hadharani basi inafaa kumsengenya katika yale aliyodhihirisha. Tunamuomba Allaah usalama.

Swali: Mtu anaweza kumsema…

Jibu: Hata baada ya kufa kwake kunapokuwa na haja ya kufanya hivo. Kwa lengo watu wasidanganyike naye.

[1] Ahmad (6/38), al-Bukhaariy (6032) na Muslim (2591).

[2] Ameipokea al-Bukhaariy (1367) na Muslim (949).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23200/ما-صحة-حديث-لا-غيبة-لفاسق
  • Imechapishwa: 25/11/2023