Swali: Wako wanazuoni wanaosema bora hii leo msafiri aswali Sunnah za Rawaatib. Ni yepi maoni yako?

Jibu: Hakuna yeyote ana haki ya kutia neno pamoja na Sunnah, ee mwanangu. Nasema kwamba hakuna yeyote ana haki ya kutia neno pamoja na Sunnah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuwa akiziswali safarini. Unapokuja mto wa Allaah basi mto wa akili unabatilika:

وَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانتَهُوا

”Kile alichokupeni Mtume basi kichukueni na kile alichokukatazeni basi kiacheni.”[1]

[1] 59:07

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23199/هل-تودى-السنن-الراتبة-في-السفر
  • Imechapishwa: 25/11/2023