Swali: Vipi tutaoanisha kati ya Hadiyth ya ´Aaishah ndani ya al-Bukhaariy:

“Msiwatukane maiti.”

na Maswahabah kumsifu maiti kwa shari[1]?

Jibu: Hapana vibaya haja ikipelekea kufanya hivo. Imekatazwa kuwatukana wafu. Isipokuwa ikiwa haja inapelekea kufanya hivo na kubainisha. Kwa mfano mtu wa Bid´ah ambaye aliacha vitabu vya kizushi ambapo mtu akawaambia watu wajihadhari vitabu vya mtu fulani. Au aliacha maneno yanayoenezwa katika magazeti na kwenginepo. Hapana neno ikiwa kuna manufaa katika kudhihirisha maovu yake.

[1] Ameipokea al-Bukhaariy (1367) na Muslim (949).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23201/ما-الضابط-في-عدم-سب-الاموات
  • Imechapishwa: 25/11/2023