Swali: Ni yepi makusudio ya mambo ya faradhi, Shari´ah, adhabu na yanayopendeza katika maneno ya ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) aliposema:

“Hakika imani ina mambo ya faradhi, Shari´ah, adhabu za Kishari´ah na yanayopendeza.”

Jibu: Ni kama alivosema ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh); mambo ya faradhi, Shari´ah, adhabu za Kishari´ah na yanayopendeza. Yote hayo yamechukuliwa ndani ya Qur-aan na Sunnah. Adhabu za Kishari´ah ni kama vile adhabu ya uzinzi, adhabu ya kunywa pombe, adhabu ya yale aliyoyaweka Allaah katika Shari´ah na adhabu ya yale aliyoyatakaza. Mambo ya Shari´ah ni vile swalah na mengine. Mambo ya faradhi yanatambulika. Mambo yanayopendeza pia yanatambulika.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23470/معنى-الفراىض-والشراىع-والحدود-والسنن
  • Imechapishwa: 28/01/2024