229 – Humraan, mtumwa wa ´Uthmaan bin ´Affaan (Radhiya Allaahu ´anh) aliyeachwa huru, ameeleza:

“Alimuona ´Uthmaan bin ´Affaan akiitisha chombo cha maji. Akajimiminia maji kwenye viganja vyake vya mikono mara tatu na kuviosha mara tatu. Kisha akaingiza mkono wake wa kushoto ndani ya chombo cha maji na kusukutua na kupalizia. Halafu akaosha uso wake mara tatu na mikono yake mpaka kwenye viwiko mara tatu. Kisha akapangusa kichwa chake na akaosha miguu yake. Halafu akasema: “Nimemuona Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akitawadha namna hii kisha akasema:

مَن توضّأَ نَحوَ وُضوئي هذا، ثم صلّى ركعتين لا يُحَدِّثُ فيهما نفسَه؛ غُفِر له ما تقدَّم من ذنبِه

“Atakayetawadha namna hii kisha akaswali Rak´ah mbili pasi na kuizungumzisha nafsi yake, atasamehewa madhambi yake yaliyotangulia.”[1]

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/211)
  • Imechapishwa: 28/01/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy