Sabuni na mafuta yanayowekwa katika baadhi ya vyakula

Swali: Je, inafaa kwa mwanamke kuweka katika nywele zake asali na yai kwa ajili ya kujipamba?

Jibu: Sijui kuhusu jambo hilo. Anajipamba kwa kuweka asali? Hapana neno ikiwa ni kwa njia ya kujipamba. Haitojuzu ikiwa ni kwa njia ya kukidharau, kucheza na chakula na israfu. Lakini ikiwa ni kwa njia ya kutibu nywele au kutibu ngozi ya nywele ambayo ina kitu ambacho kinahitaji asali au yai… ni kama ambavo kunafanywa mambo mengine kwa ajili ya matibabu. Katika hali hiyo hakuna neno.

Swali: Katika baadhi ya maduka wanasema kuwa sabuni fulani ina yai.

Ibn Baaz: Yaani imechanganywa na yai?

Muulizaji: Ndio, imechanganywa na yai.

Ibn Baaz: Haidhuru. Ni kama ambavo watu wanajitibu kwa unga na kuweka juu ya kidonda unga au wanaweka juu ya kidonda kitu kingine kwa ajili ya haja. Ni kama ambavo kunawekwa aina nyenginezo vya vyakula kwa ajili ya kujitibu. Ikiwa ni kwa njia ya kujitibu au kuzipamba nywele kama mfano wa kuweka asali kwenye nywele kwa sababu inazinufaisha nywele au akaweka yai kwa sababu yanazinufaisha nywele ikiwa katika kufanya hivo kuna faida ni sahali. Hata hivyo haijuzu ikiwa ni kucheza na neema.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23451/حكم-وضع-العسل-والبيض-على-الشعر-للتجمل
  • Imechapishwa: 28/01/2024