63. Hadiyth ”Mtume wa Allaah alitujia… ”

63 – ´Abdullaah bin Maslamah ametuhadithia, kutoka kwa Maalik, kutoka kwa Nu´aym bin ´Abdillaah al-Mujmir, ambaye ameeleza kuwa Muhammad bin ´Abdillaah bin Zayd al-Answaariy – ´Abdullaah bin Zayd ndiye ambaye aliona adhaana usingizini – amemuhadithia kutoka kwa Abu Mas´uud al-Answaaariy, ambaye amesema:

”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitujia kwenye kikao cha Sa´d bin ´Ubaadah. Bashiyr bin Sa´d akasema: ”Allaah ametuamrisha kukuswalia, ee Mtume wa Allaah. Tunakuswalia vipi?” Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akanyamaza mpaka tukatamani asingemuuliza. Kisha Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Semeni:

اللهم صل على محمد  النَّبِيّ الأُمِّيّ و على آل محمد كما صليت على إبراهيم و آل إبراهيم. و بارك على محمد  النَّبِيّ الأُمِّيّ و على آل محمد كما باركت على إبراهيم وآل إبراهيم، إنك حميد مجيد

“Ee Allaah! Msifu Muhammad na jamaa zake Muhammad kama kama Ulivyowasifu jamaa zake Ibraahiym. Na mbariki Muhammad na jamaa zake Muhammad kama Ulivyowabariki jamaa zake Ibraahiym katika ulimwengu kote. Kwani hakika Wewe ni Mwenye kuhidimiwa na Mwenye kutukuzwa.”[1]

[1] Cheni ya wapokezi ni Swahiyh kwa mujibu wa sharti za al-Bukhaariy na Muslim. Ameipokea katika “as-Swahiyh” kupitia njia nyingine kutoka kwa Maalik. Abu Daawuud (980) ameipokea kwa cheni ya wapokezi ya mtunzi.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 61-62
  • Imechapishwa: 28/01/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy