62 – Yahyaa al-Himaaniy ametuhadithia: Hushaym ametuhadithia: Abu Balj ametuhadithia: Yuunus, mtumwa wa Banuu Haashim aliyeachwa huru, amenihadithia:

”Nilimwambia ´Abdullaah bin ´Amr, au Ibn ´Umar: ”Mnamswalia vipi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?” Akasema: ”Ee Allaah! Weka sifa Zako, baraka Zako na rehema Zako kwa bwana wa waislamu, kiongozi wa wachaji na Nabii wa mwisho Muhammad, mja na Mtume Wako; kiongozi na mwongozaji wa kheri na Mtume wa rehema. Ee Allaah, mfikishe daraja yenye kusifiwa ambayo watamuonea wivu kwayo wa mwanzo na wa mwisho. Msifu Muhammad, jamaa zake Muhammad kama Ulivyomsifu Ibraahiym na jamaa zake Ibraahiym.”[1]

[1] Cheni ya wapokezi ni dhaifu. Yuunus, mtumwa wa Banuu Haashim aliyeachwa huru, simjui. Abu Balj jina lake ni Yahyaa bin Sulaym au Yahyaa bin Abiy Sulaym. Ni mwenye kuaminika, lakini wakati mwingine inatokea akakosea. Yahyaa bin ´Abdil-Hamiyd al-Himaaniy alituhumiwa kuiba Hadiyth.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 60-61
  • Imechapishwa: 28/01/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy