61 – ´Aaswim bin ´Aliy ametuhadithia: al-Ma´suudiy ametuhadithia, kutoka kwa ´Awn bin ´Abdillaah, kutoka kwa Abu Faakhitah, kutoka al-Aswad, kutoka kwa ´Abdullaah, ambaye amesema:

”Mkimswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), basi mswalieni vizuri. Kwani hamjui pengine hilo likadhihirishwa kwake.” Wakasema: ”Tufunze.” Semeni: ”Ee Allaah! Msifu, umrehemu na umbariki kiongozi wa Mitume, kiongozi wa wachaji na Nabii wa mwisho Muhammad, mja na Mtume Wako; kiongozi na mwongozaji wa kheri na Mtume wa rehema. Ee Allaah, mfikishe daraja yenye kusifiwa ambayo watamuonea wivu kwayo wa mwanzo na wa mwisho. Ee Allaah! Msifu Muhammad, jamaa zake Muhammad kama Ulivyomsifu Ibraahiym na jamaa zake Ibraahiym. Kwani hakika Wewe ni Mwenye kuhidimiwa na Mwenye kutukuzwa. Ee Allaah! Mbariki Muhammad, jamaa zake Muhammad kama Ulivyombariki Ibraahiym na jamaa zake Ibraahiym. Kwani hakika Wewe ni Mwenye kuhimidiwa na Mwenye kutukuzwa.”

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 59-60
  • Imechapishwa: 28/01/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy