Swali: Watu wengi wanaingia siku ya ijumaa wakati imamu anatoa Khutbah bila kuswali swalah ya mamkuzi ya msikiti. Je, imamu awakemee…

Jibu: Sunnah ni kwamba wanatakiwa kuswali. Ambaye anaingia na imamu anatoa Khutbah anatakiwa kuswali swalah ya mamkuzi ya msikiti. Ni lazima kwa imamu kuwakumbusha. Kwa ajili hiyo wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipomuona bwana mmoja aliyeingia na hakuswali swalah ya mamkuzi ya msikiti alimwambia:

“Simama na uswali Rak´ah mbili.”

Aliyafanya hayo (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na huku anatoa Khutbah.

Swali: Ni wengi wanaofanya hivo. Amkumbushe kila mmoja anayeingia?

Jibu: Hapana, akumbushe kwa ujumla na watajua – Allaah akitaka. Kwa mfano awaambie kwamba anayeingia msikitini basi anapaswa kuswali Rak´ah mbili. Haijalishi kitu hata kama imamu anakhutubu awakumbushe mpaka lifike jambo la Allaah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22722/حكم-تحية-المسجد-اثناء-خطبة-الجمعة
  • Imechapishwa: 02/08/2023