Swali: Je, kumepokelewa chochote juu ya muda wa kisimamo cha siku ya Qiyaamah?
Jibu: Siku ambayo ni sawa na miaka elfu khamsini. Lakini, kama alivosema Allaah (Jalla wa ´Alaa), haitofika nusu ya mchana isipokuwa atakuwa amemaliza kuhukumu kati ya watu:
أَصْحَابُ الْجَنَّةِ يَوْمَئِذٍ خَيْرٌ مُّسْتَقَرًّا وَأَحْسَنُ مَقِيلًا
“Watu wa Peponi Siku hiyo wako katika makazi bora ya kutulia na mahali pazuri kabisa pa kupumzikia.”[1]
Wanazuoni wamenyofoa hukumu hapa kwamba haitofika nusu ya mchana isipokuwa atakuwa amekwishamaliza kazi.
[1] 25:24
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22724/ما-مقدار-يوم-القيامة-والموقف-فيه
- Imechapishwa: 02/08/2023