Imamu kuja mapema siku ya ijumaa na kusubiri swalah

Swali: Imamu kusubiri swalah?

Jibu: Anatakiwa kuchunga wakati unaofaa ili asiwatie watu uzito.

Swali: Nakusudia kwamba fadhilah za yeye kutangulia?

Jibu: Akitangulia msikitini hapana vibaya. Mtume (Swalla Allaahu ´´alayhi wa sallam) alikuwa akitoka wakati wa swalah. Lakini akiona kuwa manufaa ni yeye kutangulia msikitini hapana vibaya. Sijui kikwazo chochote.

Swali: Lakini kwa ajili ya kutafuta fadhilah hizi?

Jibu: Hapana neno. Kunatarajiwa kwake kheri.

Swali: Je, imesihi kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akija kabla ya kukimiwa?

Jibu: Sijafikiwa na chochote kuhusu hilo. Hata hivyo hapana vibaya. Hadiyth zinafahamisha ya kwamba ambaye atakuja mapema yuko na kheri kubwa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23727/هل-يشرع-للامام-انتظار-الصلاة-بالمسجد
  • Imechapishwa: 13/04/2024