Imamu aliyekula vitungu saumu na vitunguu maji kuwaswalisha watu

Swali: Inafaa kwa imamu kuwaswalisha watu akiwa amekula vitungu saumu?

Jibu: Hukumu inamgusa imamu na wengine. Imamu jambo lake linakuwa baya zaidi. Imamu anapaswa awe ruwaza njema kwa watu. Kwa hivyo haitakiwi kwake kufanya hivo. Kitu hicho hakifai kwa imamu wala maamuma. Haijuzu kwa mtu kula kitungu saumu wala kitunguu maji kisha akaingia msikitini. Ni mamoja akawa ni imamu au maamuma. Imamu anatakiwa awe kiigizo chema kwa watu. Ni vipi yeye anafanya hivo?

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (21)
  • Imechapishwa: 20/08/2021