Swali: Katika nchi yetu pahali pa makaburi hapako kwa mujibu wa Shari´ah. Je, inajuzu kuwazikaeko maiti?

Jibu: Vipi hayako kwa mujibu wa Shari´ah? Sio makaburi ya waislamu? Muislamu anatakiwa kuzikwa kwenye makaburi ya waislamu pasi na kujali mahala; katika nchi za makafiri na nchi za waislamu. Ikiwa waislamu wana pahala pa kuzikia azikwe huko. Na ikiwa hawana pahala pa kuzikia basi asizikwe katika makaburi ya makafiri. Katika hali hiyo asafirishwe.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fath-il-Majiyd (30) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/fathul%20majd%20-%2019%20-%2010-%20-1436.mp3
  • Imechapishwa: 12/02/2017