Msimamo kwa mzushi ambaye Bid´ah zake ni kufuru

Swali: Vipi mtu atatangamana na mtu wa Bid´ah ambaye Bid´ah zake ni kufuri? Je, inajuzu kumsusa?

Jibu: Bila ya shaka. Ikiwa hatoacha Bid´ah zake ni wajibu kumsusa na kujiepusha naye.

Lakini ni nani atayehakikisha hili? Baadhi ya ndugu wanaonelea kila kitu ambacho ni wajinga kwacho kuwa ni Bid´ah. Ni lazima kuhakikishwe kuwa kweli ni Bid´ah na kuwepo dalili. Baadhi ya ndugu wanafanyiana Tabdiy´ wao kwa wao pasi na dalili. Wanafanya hivo kwa sababu hawaonelei sawa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fath-il-Majiyd (30) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/fathul%20majd%20-%2019%20-%2010-%20-1436.mp3
  • Imechapishwa: 12/02/2017