Ibn ´Uthaymiyn kuhusu hukumu ya kuchinja katika ´Iyd-ul-Adhwhaa

Kuchinja katika ´Iyd-ul-Adhwhaa ni jambo limependekezwa mno. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alidumu juu yake na akachinja miaka kumi na akahimiza juu ya kitendo hicho mpaka akafikia kusema:

“Yule mwenye nafasi na asichinje basi asisogelee uwanja wetu wa kuswalia.”[1]

Alikuwa akidhihirisha kitendo hicho kama vile ni moja ya nembo za Uislamu. Alikuwa anatoka na vichinjwa vyake kwenda katika uwanja wa kuswalia na akivichinja huko. Kwa ajili hii wanachuoni wametofautiana kama ni jambo lililopendekezwa au jambo la lazima.

Abu Haniyfah (Rahimahu Allaah) na wafuasi wake wakasema kuwa ni jambo la lazima na kwamba yule mwenye uwezo anapata dhambi asipochinja. Shaykh-ul-Islaam ameegemea katika maoni haya kwa sababu ni nembo ya Uislamu ambayo imeambatanishwa na swalah pale aliposema (Ta´ala):

فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَانْحَرْ

”Basi swali kwa ajili ya Mola wako na [pia ukichinja] na chinja [kwa ajili Yake]!”[2]

قُلْ إِنَّ صَلَاتِي وَنُسُكِي وَمَحْيَايَ وَمَمَاتِي لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ

”Sema: “Hakika swalah yangu na kichinjwa changu na uhai wangu na kufa kwangu ni kwa ajili ya Allaah pekee, Mola wa walimwengu.”[3]

Maoni yanayosema kuwa ni lazima kwa yule mwenye uwezo yana nguvu sana kutokana na wingi wa dalili ambazo dini imetilia mkazo kitendo hicho.

[1] Ahmad (1/321), Ibn Maajah (3123), ad-Daaraqutwniy (2/545) na al-Haakim (4/231).

[2] 108:2

[3] 6:162

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ash-Sharh al-Mumti´ (7/517-518)
  • Imechapishwa: 11/07/2020