Ibn Taymiyyah kuhusu hukumu ya kuchinja katika ´Iyd-ul-Adhwhaa

Kuhusu kuchinja katika ´Iyd-ul-Adhwhaa kwa mujibu wa maoni sahihi zaidi ni kwamba ni lazima. Kitendo hicho ni miongoni mwa desturi kubwa za Uislamu, ni kichinjwa chenye kuenea katika miji yote wa na pia ni kichinjwa kilichoambatana na swalah pale Allaah aliposema:

قُلْ إِنَّ صَلَاتِي وَنُسُكِي وَمَحْيَايَ وَمَمَاتِي لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ

”Sema: “Hakika swalah yangu na kichinjwa changu na uhai wangu na kufa kwangu ni kwa ajili ya Allaah pekee, Mola wa walimwengu.”[1]

فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَانْحَرْ

”Basi swali kwa ajili ya Mola wako na [pia ukichinja] na chinja [kwa ajili Yake]!”[2]

Ameamrisha kuchinja kama alivyoamrisha kuswali. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَلِكُلِّ أُمَّةٍ جَعَلْنَا مَنسَكًا لِّيَذْكُرُوا اسْمَ اللَّـهِ عَلَىٰ مَا رَزَقَهُم مِّن بَهِيمَةِ الْأَنْعَامِ ۗ فَإِلَـٰهُكُمْ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ فَلَهُ أَسْلِمُوا ۗ وَبَشِّرِ الْمُخْبِتِينَ

“Na kwa kila Ummah Tumeweka taratibu za ‘ibaadah ili wataje jina la Allaah kwa yale aliyowaruzuku katika wanyama hoa. Kwa hiyo mwabudiwa wenu wa haki ni Mungu Mmoja pekee, basi Kwake jisalimisheni! Na wabashirie wanyenyekevu.”[3]

وَالْبُدْنَ جَعَلْنَاهَا لَكُم مِّن شَعَائِرِ اللَّـهِ لَكُمْ فِيهَا خَيْرٌ ۖ فَاذْكُرُوا اسْمَ اللَّـهِ عَلَيْهَا صَوَافَّ ۖ فَإِذَا وَجَبَتْ جُنُوبُهَا فَكُلُوا مِنْهَا وَأَطْعِمُوا الْقَانِعَ وَالْمُعْتَرَّ ۚ كَذَٰلِكَ سَخَّرْنَاهَا لَكُمْ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ لَن يَنَالَ اللَّـهَ لُحُومُهَا وَلَا دِمَاؤُهَا وَلَـٰكِن يَنَالُهُ التَّقْوَىٰ مِنكُمْ ۚ كَذَٰلِكَ سَخَّرَهَا لَكُمْ لِتُكَبِّرُوا اللَّـهَ عَلَىٰ مَا هَدَاكُمْ ۗ وَبَشِّرِ الْمُحْسِنِينَ

“Na ngamia na ng’ombe Tumekufanyieni kuwa ni miongoni mwa nembo za Allaah, kwavyo mnapata kheri nyingi. Hivyo basi litajeni jina la Allaah juu yao wanapopangwa safu [wakati wa kuchinjwa]; na waangukapo ubavu, basi kuleni kutoka humo na lisheni waliokinai [kwa kile kichache walichonacho] na wanaolazimika kuomba. Hivyo ndivyo tulivyowatiisha kwa ajili yenu – ili mpate kushukuru. [Wanyama hao mnaochinja] haimfikii Allaah nyama zake wala damu yake, lakini inamfikia uchaji kutoka kwenu. Hivyo ndivyo tulivyowatiisha kwenu ili mpate kumtukuza Allaah kwa yale aliyokuongozeni na wabashirie watendao wema.”[4]

Pia kitendo hicho ni miongoni mwa dini ya Ibraahiym ambayo tumeamrishwa kuifuata. Isitoshe kupitia kitendo hicho kunakumbukwa kisa cha Ibraahiym kumchinja Ismaa´iyl. Ni vipi basi itafaa kwamba waislamu wote waache jambo hilo? Kufanya kuchinja ni jambo la khatari kuliko kuacha kuhiji kwa miaka kadhaa.

[1] 6:162

[2] 108:2

[3] 22:34

[4] 22:36-37

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (23/162)
  • Imechapishwa: 11/07/2020