al-Mardaawiy kuhusu hukumu ya kuchinja katika ´Iyd-ul-Adhwhaa

Ni jambo limekokotezwa sana kuchinja ´Iyd-ul-Adhwhaa. Haya ndio maoni ya madhehebu pasi na mashaka yoyote. Hanaabilah wengi wana maoni mengine na yamesemwa na Ahmad. Wengi wao wanaona kuwa ni jambo la kukata. Mtunzi wa “ar-Ri´aayah” amesema:

“Imechukizwa kuacha kuchinja ikiwa mtu ana uwezo. Ndivo alivosema Ahmad.”

Ahmad anayo maoni mengine yanayosema kuwa ni lazima akiwa mtu ni tajiri. Wengi wameyapokea.

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin Sulaymaan al-Mardaawiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Inswaaf (4/105)
  • Imechapishwa: 11/07/2020