Ibn Baaz kuhusu ujinga ni udhuru 1

Swali: Ni ipi hukumu kwa asiyejua Tawhiyd. Anaomba badala ya Allaah na yeye anaswali na kufunga?

Jibu: Yule ambaye anamshirikisha Allaah na yeye yuko kati ya Waislamu, huyu hukumu yake ni ya washirikina. Ni wajibu kwake kujifunza. Ni wajibu kwake kumcha Allaah na aulize. Maadamu anaishi kati ya Waislamu na anaomba watu wa makaburi [maiti] – anamshirikisha Allaah – yeye ni pamoja na washirikina. Ama akiwa katika mji ambapo hakujafika Da´wah, Qur-aan wala Sunnah, huyu hukumu yake ni kama ya Ahl-ul-Fatrah. Jambo lake anaachiwa Allaah siku ya Qiyaamah. Sio katika Waislamu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=12780
  • Imechapishwa: 03/05/2015