Swali: Tunatarajia kutoka kwako kuwatanabahisha kina dada ambao ni Waislamu ajinabi kutilia umuhimu Hijaab ya Kishari´ah na khaswa katika Haraam. Kwa kuwa sisi wanaume tunaudhika na tunakhofia fitina kutokana na kitendo hichi. Hali kadhalika tunaomba uwatanabahishe Swalah hili wale ambao wana majukumu juu ya jambo hili Haramayn [Makkah na al-Madiynah]. Uwatanabahishe pia wanawake hukumu ya Swalah kwa yule ambaye miguu yake inaonekana, uso wake na mikono yake mbele ya wanaume.

Jibu: Tunawausia dada zetu kwa ajili ya Allaah kujisitiri na kujiweka mbali na fitina. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

وَقَرْنَ فِي بُيُوتِكُنَّ وَلَا تَبَرَّجْنَ تَبَرُّجَ الْجَاهِلِيَّةِ الْأُولَىٰ

“Bakieni majumbani mwenu na wala msijishauwe mshauwo wa wanawake majahili wa mwanzo.” (33:33)

Kuswali nyumbani kwao ni bora zaidi. “at-Tabarruj” maana yake ni kuonekana mapambo na vile vinavyofitinisha. Allaah kakataza hilo. Vilevile amesema (Jalla wa ´Alaa):

وَإِذَاسَأَلْتُمُوهُنَّ مَتَاعًا فَاسْأَلُوهُنَّ مِن وَرَاءِ حِجَابٍ ۚ ذَٰلِكُمْ أَطْهَرُ لِقُلُوبِكُمْ وَقُلُوبِهِنَّ

“Mnapowauliza haja, basi waulizeni nyuma ya pazia. Hivyo ni utwaharifu zaidi kwa nyoyo zenu na nyoyo zao.” (33:53)

Lililo la wajibu kwao ni kujisitiri mwili wao wote; nyuso zao, viganja vyao vya mikono na miguu yao. Ni wajibu kujisitiri mbele ya wanaume katika msikiti huu na mingine. Vilevile kwenye masoko. Ni wajibu kujisitiri ili asiwafitinishe watu na akaja kuwadhuru. Hili ni khatari na shari yake ni kubwa. Hivyo ni wajibu kutahadhari na hilo. Ima aswali nyumbani kwake – na hili ndio bora – au ajihifadhi kwenye Msikiti huu na mingine na awe ni mwenye kujisitiri mwili wake wote mbele ya wanaume, uso wake, mikono, miguu na vinginevyo. Awe ni mwenye kujisitiri na Hijaab kuwaepusha watu na fitina. Tunaomba uongofu kwa Allaah kwa watu wote.

Tunawausia vilevile wale ambao wana majukumu katika Msikiti huu Mtukufu watilie umuhimu suala hili na wawanasihi wanawake kutoleta sababu za fitina.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=12780
  • Imechapishwa: 03/05/2015