Ibn Baaz kuhusu mnyonyeshaji na mjamzito kutofunga Ramadhaan

Swali: Mwenye kunyonyesha akikhofia juu ya mtoto wake au juu ya nafsi yake na asifunge Ramadhaan na baada ya Ramadhaan akalipa siku zake alizokula na hakulisha masikini. Je, Swawm yake ni sahihi au ni lipi linalomuwajibikia?

Jibu: Kauli sahihi ni kwamba atalipa siku zake na hana juu yake kulisha chakula. Akila kwa ajili ya mtoto wake, bi maana akifunga hatopata maziwa au akala kwa ajili ya mimba au maradhi, atalipa tu na hana juu yake chakula.

Baadhi ya wanachuoni wamesema kuwa atalisha pia ikiwa kula kwake ilikuwa ni kwa sababu ya mtoto, lakini sahihi ni kwamba atalipa na hana juu yake kitu. Atalipa na himdi zote ni za Allaah. Kwa kuwa Allaah (Ta´ala) Anasema:

وَمَن كَانَ مَرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ

“Na atakayekuwa mgonjwa au safarini basi (atimize) idadi katika siku nyinginezo.” (02:285)

Vilevile Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimpa rukhusa mjamzito na anayenyonyesha na hakusema kuwa watalisha chakula pia. Mwenye ujauzito na anayenyonyesha wakila kwa sababu ya uzito, ni kama mfano wa mgonjwa. Watalipa tu na hawana juu yao kitu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=12827
  • Imechapishwa: 05/05/2015