Swali: Mimi ni mwanamke nimeolewa. Nina watoto ambao nimekuwa ni mwenye subira kwa ajili yao. Mume wangu ananitukana na ananifanyia mambo ambayo yasiyomridhisha Allaah. Ninakuomba uninasihi ni lipi ninaloweza kufanya?

Jibu: Tunakunasihi kuwa na subira, matangamano mazuri, maneno mazuri na kumpa nasaha. Mwambie “Ee fulani, mche Allaah! Jikinge kwa Allaah kutokana na shaytwaan! Muogope Allaah! Usitukane!” Zungumza kwa maneno mazuri. Mnasihi. Kadhalika baba yako, kaka yako au baadhi ya watu unaojua wanamfahamu vizuri wamnasihi mpaka aweze kujirudi. Anasihiwe.

Kuwa ni mwenye subira. Ni lazima uwe ni mwenye subira. Dunia hii ni nyumba ya tabu. Hivyo ni lazima kuwa na subira pamoja na kumuombea du´aa Allaah Amuongoze. Muombee kwa Allaah katika Sujuud, mwisho wa Swalah yako kabla ya kutoa salamu na katika kila wakati. Muombe Allaah kwa kusema “Ee Allaah, muongoze! Ee Allaah, nikinge na shari yake! Ee Allaah, msamehe mume wangu! Ee Allaah, mnyooshe hali yake!” Muombe Allaah. Zungumza naye kwa maneno mazuri. Ninakubashiria kheri. Allaah (Jalla wa ´Alaa) Anasema:

وَمَن يَتَّقِ اللَّـهَ يَجْعَل لَّهُ مَخْرَجًا

“Na yeyote yule anayemcha Allaah, basi atamajaalia njia ya kutokea.” (65:02)

وَمَن يَتَّقِ اللَّـهَ يَجْعَل لَّهُ مِنْ أَمْرِهِ يُسْرًا

“Na yeyote yule anayemcha Allaah, basi atamjaalia wepesi katika jambo lake.” (65:04)

Ikiwa ni mume mwema na anaswali, basi kuwa ni mwenye subira. Ama ikiwa haswali achana naye. Kwa kuwa asiyeswali ni kafiri na tunaomba kinga kwa Allaah. Nenda mahakamani na uombe kutengana naye. Ama ikiwa anaswali lakini anapogombana na wewe anakuwa na ulimi mbaya na tabia mbaya, lakini pamoja na yote hayo ni Muislamu mzuri, mche Allaah na kuwa ni mwenye subira. Kupigana naye jihadi kwa kuzungumza naye maneno mazuri, kutangamana naye vizuri, kumpa nasaha, kumuombea kwa Allaah amuongoze na mfano wa haya.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=12827
  • Imechapishwa: 05/05/2015