Ibn Baaz juu ya kumshuhudia kafiri kwa dhati yake Moto

Swali: Je, tunaweza kusema juu ya kafiri binafsi ya kwamba amekufa katika ukafiri na yuko Motoni na Allaah Amlaani? Kwa kuwa baadhi ya watu wamekataza hili na kusema “Pengine alisilimu na wewe hukujua hilo”. Je, maneno yake ni sahihi?

Jibu: Ambaye utajua kuwa amekufa katika ukafiri, unaweza kumshahidilia ukafiri. Yule usiyejua, unasema “Allaah ndiye Anayejua zaidi”. Lakini badala yake unatakiwa kusema “Allaah Awalaani Makafiri”, “Mwenye kufa katika ukafiri yuko Motoni” kama ambavyo unaweza kusema “Atakayekufa juu ya Imani basi yuko Peponi”. Hili wamekubaliana Waislamu wote ya kwamba mwenye kufa katika Imani basi ni katika watu wa Peponi na mwenye kufa katika ukafiri basi ni katika watu wa Motoni. Unashahidilia kwa jumla.

Ama yule usiyejua hali yake na pengine alitubia, unasema “Allaah ndiye Anajua zaidi”. Matendo yake ni ya kikafiri kwa kuwa alikuwa ni kafiri, ikiwa alikufa juu yake. Na ikiwa alitubu, Allaah Anamsamehe. Yule usiyejua (hali yake wakati alipokufa) usiseme ni mtu wa Peponi wala wa Motoni. Kwa ajili hii baadhi ya wanachuoni wamesimama kwa baadhi ya watu wanaonasibishwa matendo ya kikafiri na wanasema haijulikani uhakika wao kuwa walikufa katika hayo au hapana. Lakini hata hivyo wanahukumiwa kwa matendo yao. Mwenye kumtukana Allaah ni kafiri, mwenye kuacha Swalah ni kafiri, mwenye kuabudu masanamu, mwenye kuyategemea makaburi, anawataka msaada maiti na mwenye kuwataka msaada majini ni kafiri. Ikiwa atatubu, Allaah Humsamehe. Tunasema Abu Jahl alikufa juu ya ukafiri, aliuwawa katika vita vya Badr. [Sauti haisikiki]. Abu Jahl alikufa juu ya ukafiri. Abu Lahab alikuwa juu ya ukafiri na hivyo tunawashahidilia kutokana na Hadiyth zilizokuja kutoka kwa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ama yule tusiyejua alikufa juu ya nini, Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ndiye Atakayemhukumu. Lakini tunasema kwa jumla ya kuwa, kila muumini yuko Peponi na kila kafiri yuko Motoni. Vilevile kwa jumla, Allaah Awarahamu waumini na Allaah Awalaani makafiri. Kama alivyosema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Allaah Awalaani mayahudi na manaswara, wameyafanya makaburi ya Mitume wao kuwa Misikiti.”

Akasema Allaah (Jalla wa ´Alaa):

“Basi laana ya Allaah juu ya wakanushaji.”
“Tanabahi! Laana ya Allaah iko juu ya madhalimu.”
Kwa jumla. 
“Tanabahi! Laana ya Allaah iko juu ya madhalimu.”
“Basi laana ya Allaah juu ya wakanushaji.”

“Tanabahi! Laana ya Allaah iko juu ya mafusaki.”

Kwa jumla.

“Allaah Awasamehe waumini.”

“Allaah Awarahamu waumini.”

“Allaah Awawie Radhi waumini.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=12825
  • Imechapishwa: 20/11/2014