Kuwaomba msaada na uokovu maiti ni shirki

Swali: Sisi tuko katika mji ambapo kumekithiri sanakuwaomba uokovu na kuwaomba msaadamaiti. Wanawawekea nadhiri na kuwachinjia. Wanaitakidi ya kwamba wanajua mambo ya ghaibu na wanasema:

شُفَعَاؤُنَا عِندَ اللَّـهِ

“Waombezi wetu mbele ya Allaah.” (10:18)

Unawanasihi nini? Kwa kuwa baadhi yao hivi sasa wako na sisi msikitini.

Jibu: Hii ndio Shirki kubwa. Hii ndio dini ya washirikina. Kuwaabudu maiti, kutafuta ukombozi na kuomba kinga kwa maiti, kuwawekea nadhiri na kuwachinjia, hii ndio dini ya washirikina. Hii ndio dini ya Abu Jahl na mfano wake. Hii ndio Shirki kubwa na tunaomba kinga kwa Allaah. Wanasema:

مَا نَعْبُدُهُمْ إِلَّا لِيُقَرِّبُونَا إِلَى اللَّـهِ زُلْفَىٰ

“Hatuwaabudu isipokuwa kwa lengo la kutukurubisha kwa Allaah ukaribu.” (39:03)

وَيَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَضُرُّهُمْ وَلَا يَنفَعُهُمْ وَيَقُولُونَ هَـٰؤُلَاءِ شُفَعَاؤُنَا عِندَ اللَّـهِ

“Wanaabudu asiyekuwa Allaah ambao hawawezi kuwadhuru na wala kuwanufaisha na wanasema: “Hawa ni waombezi wetu mbele ya Allaah.” (10:18)

Haya ndiyo walikuwa wakifanya washirikina na ni haya haya ndiyo yanayofanywa kwa kumuomba al-Badawiy, al-Husayn n.k. Kuwaomba Du´aa na kuwaomba ukombozi, yote haya ni katika Shirki kubwa. Wanamuomba vilevile [sauti haisikiki], Zaynab, Shaykh ´Abdul-Qaadiyr Iraaq na mfano wao. Hii ni katika Shirki kubwa. Kuwaomba waliyomo ndani ya makaburi, kuwataka ukombozi, kuwawekea nadhiri na kuwachinjia, hii ndio Shirki kubwa. Hii ndio dini ya Abu Jahl na watu mfano wake. Lililo la wajibu ni kuomba Tawbah, kujuta, kujivua na kuazimia kutorudi. Badala yake ´ibaadah afanyiwe Allaah Mmoja. Yeye ndiye Mwenye kuombwa. Seme “Allaah Nisamehe na Nirahamu”, “Ee Allaah niokoe, Allaah Ninusuru, Allaah nipe Pepo, Allaah Niokoe na Moto, Allaah Waongoze watoto wangu, Allaah Niruzuku kwa fadhila Zako n.k.” Muombe Mola Wako. Usiwaombe mawalii, Malaika na wengineo. Allaah Kasema:

وَقَالَ رَبُّكُمُ ادْعُونِي أَسْتَجِبْ لَكُمْ

“Na Mola wenu Amesema: “Niombeni, Nitakuitikieni.” (40:60)

وَإِذَا سَأَلَكَ عِبَادِي عَنِّي فَإِنِّي قَرِيبٌ ۖ أُجِيبُ دَعْوَةَ الدَّاعِ إِذَا دَعَانِ

“Watakapokuuliza waja Wangu kuhusu Mimi, basi Mimi niko karibu Naitikia maombi ya muombaji anaponiomba.” (02:186)

فَلَا تَدْعُ مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ فَتَكُونَ مِنَ الْمُعَذَّبِينَ

”Basi usiombe pamoja na Allaah mungu mwengine ukaja kuwa miongoni mwa watakaoadhibiwa.” (26:213)

Anamwambia pia Mtume Wake:

وَلَا تَدْعُ مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَنفَعُكَ وَلَا يَضُرُّكَ ۖ فَإِن فَعَلْتَ فَإِنَّكَ إِذًا مِّنَ الظَّالِمِينَ

“Na wala usiombe badala ya Allaah asiyekufaa [ukimwabudu] na wala asiyekudhuru [usipomwabudu]. Na ukifanya hivyo, basi hakika utakuwa miongoni mwa madhalimu.” (10:106)

yaani miongoni mwa washirikina. Anasema tena (Subhaanahu):

ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمْ لَهُ الْمُلْكُ ۚ وَالَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِهِ مَا يَمْلِكُونَ مِن قِطْمِيرٍ إِن تَدْعُوهُمْ لَا يَسْمَعُوا دُعَاءَكُمْ وَلَوْ سَمِعُوا مَا اسْتَجَابُوا لَكُمْ ۖ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ يَكْفُرُونَ بِشِرْكِكُمْ ۚ وَلَا يُنَبِّئُكَ مِثْلُ خَبِيرٍ

“Huyo basi Ndiye Allaah Mola wenu, ufalme ni Wake pekee. Na wale mnaowaomba badala Yake hawamiliki hata kijiwavu cha kokwa ya tende. Mkiwaomba, hawasikii maombi yenu, na hata wakisikia, basi [wasingeliweza] kukujibuni na Siku ya Qiyaamah watakanusha ushirikina wenu na wala hakuna atakayekujulisha kama Mjuzi wa khabari zote za ndani.” (35:13-14)

وَمَن يَدْعُ مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ لَا بُرْهَانَ لَهُ بِهِ فَإِنَّمَا حِسَابُهُ عِندَ رَبِّهِ ۚ إِنَّهُ لَا يُفْلِحُ الْكَافِرُونَ

“Yeyote yule anayeomba pamoja na Allaah mungu mwengine hana ushahidi wa wazi wa hilo; basi hakika hesabu yake iko kwa Mola wake. Hakika hawafaulu makafiri.” (23:117)

Ameita kuwa ni kufuru kubwa.

إِنَّهُ لَا يُفْلِحُ الْكَافِرُونَ

“Hakika hawafaulu makafiri.” (23:117)

Ameita kumuomba asiyekuwa Allaah, sawa ikiwa ni majini au mawalii, Amewaita kuwa ni makafiri. Lililo la wajibu ni kuwa na tahadhari na kuwabainishia watu hawa Tawhiyd na Kuwawekea dalili wazi na kuwatahadharisha na shirki hii.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=12825
  • Imechapishwa: 20/11/2014