Swali: Vijana wengi wanatumia hoja ya kwamba kutopata idhini kutoka kwa mzazi [wakati wa kwenda katika Jihaad] ni dhambi tu na shahidi anasamehewa pale ambapo tone lake tu la kwanza linapotonya. Vipi mtu atamraddi?

Jibu: Huyu sio shahidi. Huyu ni mfanya dhambi. Huyu sio shahidi bali kinyume chake ni mfanya dhambi. Utokaji huu haukubaliki Kishari´ah. Vipi atakuwa ni shahidi na utokaji wake haukubaliwi na Shari´ah?

Watu hawa ni kama nilivyowaambia. Wanachukua baadhi ya dalili na wanaacha zingine. Huu ndio mfumo wa Khawaarij na ni mfumo wa watu wapotevu ambao wanachukua dalili zisizokuwa wazi na wanaacha zilizo wazi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Buluugh al-Maraam (09) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/14705
  • Imechapishwa: 19/04/2015