Tofauti ya Jihaad ya kujihami na ya kushambulia

Swali: Tunaomba utuwekee wazi tofauti kati ya Jihaad ya kujihami  [Jihaad-ul-Daf´iy] na Jihaad ya kushambulia [Jihaad-ut-Twalab]?

Jibu: Jihaad ya kujihami ni pale ambapo maadui wanapovamia mji wa Waislamu. Katika hali hii ni wajibu kwa kila mwenye uwezo apambane. Vilevile hili linatumika katika Jihaad ya kushambulia pale ambapo watakuwa wameshaingia uwanjani. Katika hali hii itakuwa haijuzu kwake kukimbia kutoka uwanjani. Bali ni wajibu kwako kupambana. Hii ndio Jihaad ya kujihami.

Lakini kuhusu Jihaad ya kushambulia ni kuwashambulia maadui katika miji yao. Wao hawakuja katika miji yetu, bali sisi ndio tunawapiga vita katika miji yao. Hii ndio Jihaad ya kushambulia.

Jihaad ya kujihami ni faradhi kwa watu wote. Ni faradhi kwa kila Muislamu mwenye uwezo [wa kupambana]. Ama kuhusu Jihaad ya kushambulia ni faradhi kwa baadhi ya watu. Wakitoka na wakaenda baadhi ya watu inakuwa sio wajibu kwa wengine.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Buluugh al-Maraam (09) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/14705
  • Imechapishwa: 19/04/2015