Swali: Ni yapi maoni yako kwa mwenye kumuuliza mwanachuoni kuhusu jambo fulani kisha baada ya hapo anaenda kwa mwanachuoni mwingine na kumuuliza kuhusu jambo hilo hilo?

Jibu: Huyu ni mchezaji. Huyu anataka kuchezesha majibu. Pengine ana makusudio mabaya anachotaka ni kuangalia majibu tofauti watayotoa wanachuoni na halafu baada ya hapo aseme mwanachuoni fulani amesema hivi na huyu amesema vile. Haijuzu kufanya hivi kamwe.

Kwanza unapotaka kuuliza usiuleze mtu yoyote. Muulize yule mtu unayeamini elimu na Dini yake na amepewa kazi ya Fatwa. Muulize huyu. Baada ya hapo chukua jibu lake na usiende kuuliza kwa mtu wa pili na wa tatu. Chukua maoni ya aliyekujibu midhali mtu huyo ni katika wanachuoni na wachaji Allaah:

فَاسْأَلُواْ أَهْلَ الذِّكْرِ إِن كُنتُمْ لاَ تَعْلَمُونَ

“Basi waulizeni wenye ukumbusho kama nyinyi hamjui.” (16:43)

Watu wenye ukumbusho ndio wenye kustahiki kuulizwa. Wana elimu na uchaji Allaah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Buluugh al-Maraam (36) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/blug–1431-08-15.mp3
  • Imechapishwa: 21/04/2015