Swali: Ni ipi hukumu ya kuhukumiana kwa wazee wa makabila ili kutatua mizozo ilioko kati ya makabila kwa sababu wakati mwingine wanahukumu kinyume na Aliyoteremshwa Allaah?

Jibu: Si kwamba wanafanya hivi wakati fulani. Wao siku zote huhukumu kinyume na Aliyoteremsha Allaah kwa sababu ni wajinga. Hawajui yale Aliyoteremsha Allaah. Mmesikia ya kwamba mtu akihukumu pasina elimu anaingia Motoni hata kama atapatia. Allaah (Jalla wa ´Alaa) Amesema:

أَفَحُكْمَ الْجَاهِلِيَّةِ يَبْغُونَ ۚ وَمَنْ أَحْسَنُ مِنَ اللَّـهِ حُكْمًا لِّقَوْمٍ يُوقِنُونَ

“Je, wanataka hukumu za kipindi cha kijahili? Na nani mbora zaidi kuliko Allaah katika kuhukumu kwa watu wenye yakini.”[1]

Hizi ni katika hukumu za kijahiliyyah. Kuhukumiana kwa kanuni za kimakabila na mambo ya kiurithi ni hukumu za kijahiliyyah. Haijuzu kuhukumu isipokuwa kwa kutumia Qur-aan na Sunnah. Himdi zote ni za Allaah Saudi Arabia kuna mahakama ya Kishari´ah katika kila kijiji na kila mji. Hayakosekani. Vipi basi mtu aende kuhukumiana kikabila ilihali kuna mahakama za Kishari´ah? Hili halijuzu.

[1] 5:50

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Buluugh al-Maraam (36) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/blug–1431-08-15.mp3
  • Imechapishwa: 21/04/2015