Huyu ndiye mbora wa watu mbele ya Allaah

Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliulizwa kuhusu mtu bora mbele ya Allaah ambapo (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akajibu:

“Hakika mbora katika watu ni yule anayemcha Allaah zaidi.”

Ikiwa unataka kuwa mbora zaidi mbele ya Allaah, basi ni juu yako kumcha Allaah. Kila ambavyo mtu atakuwa na uchaji Allaah zaidi, basi ndivyo ambavyo anakuwa mbora zaidi mbele ya Allaah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/523)
  • Imechapishwa: 27/06/2023