Huyu anaingia katika fadhilah za kumtazama yatima?

Swali: Kuhusiana na suala la kumtazama yatima; inatokea wakati mwingine kuna kuponi ya kuwatazama mayatima kwa kipindi cha mwaka mmoja au miaka kadhaa. Je, mtu anaingia katika Hadiyth[1] ikiwa atamfadhili kwa kipindi cha mwaka mmoja peke yake?

Jibu: Kunatarajiwa kwake kheri – Allaah akitaka. Ikiwa atachangia katika kheri hii basi kunatarajiwa kwake kheri.

[1] Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Mimi na mwenye kumtazama yatima huko Peponi tuko hivi. Akaashiria vidole vyake; cha shahaadah na cha kati na kuvipambanua baina yake kiasi fulani.” (al-Bukhaariy 5304).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21631/هل-يشمل-فضل-كفالة-اليتيم-الكفالة-الموقتة
  • Imechapishwa: 04/09/2022