Huu ni utovu wa adabu kwa Mtume (´alayhis-Salaam)          

Swali: Je, inaingia katika kunyanyua sauti juu ya sauti ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambako kumekatazwa[1] kunyanyua sauti kwa yule anayesoma Hadiyth ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?

Jibu: Ndio. Huku ni kuwa na utovu wa adabu kwa Hadiyth za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ukisikia Hadiyth kaa kimya kwa kuwa anakuzungumzisha wewe na wewe ni mwenye haja kwake. Vipi unatoka kwake na kunyanyua sauti juu yake? Miongoni mwa adabu na Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni wewe kukaa kimya wakati kunaposomwa Hadiyth kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

[1] 49:02

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (03) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1427-2-13.mp3
  • Imechapishwa: 19/08/2020