Tafsiyr za Qur-aan ambazo al-Fawzaan anapendekeza

Swali: Ni Tafsiyr ipi iliyosalimika na makosa ambayo unapendekeza?

Jibu: Tafsiyr zilizosalimika na makosa ni nyingi – na himdi zote ni za Allaah. Kubwa na pana katika hizo ni “Tafsiyr Ibn Jariyr” ambaye ndio imamu wa wafasiri wa Qur-aan. Kila aliyekuja baada yake ananukuu kutoka kwake. Kisha kunakuja “Tafsiyr Ibn Kathiyr”, “Tafsiyr al-Baghawiy”, “Tafsiyr as-Sa´diy” ya leo, “Tafsiyr ya Shaykh wetu Muhammad Amiyn ash-Shanqiytwiy. Zote hizi ni – na himdi zote ni za Allaah – Tafsiyr zenye kuaminika zilizojengewa juu ya dalili na juu ya maneno y Salaf.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (03) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1427-2-13.mp3
  • Imechapishwa: 19/08/2020