Hukumu ya mwenye kutanguliza Sa´y kabla ya Twawaaf

Swali: Vipi ikiwa mwanamke atatanguliza Sa´y kabla ya Twawaaf?

Jibu: Kilichopendekezwa ni kwamba abaki hadi atakapoweza kutufu kwanza, kwa sababu Sa´y inapaswa kufanyika baada ya Twawaaf. Hata hivyo inasihi kwa mujibu wa maoni yenye nguvu. Lakini kilichowekwa katika Shari´ah ni kwamba abaki hadi atakapotwahirika, kisha baada ya hapo atufu na kufanya Sa´y. Imesihi kutoka kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba aliulizwa:

”Ee Mtume wa Allaah, nimefanya Sa´y kabla ya kutufu?” Akasema: ”Hakuna shida.”

Hata hivyo Sunnah ni kwamba muumini atufu kwanza kisha afanye Sa´y, kama alivyofanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kuhusu mwanamke aliye katika hedhi, anapaswa kubaki hadi atakapotwaharika. Akishatwahirika atafanya Twawaaf na Sa´y.

Swali: Je, Hadiyth inayohusu mtu aliyeuliza swali hilo ni maalum na mtu aliyetanguliza Sa´y katika hajj peke yake?

Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakumpambanulia muulizaji.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24987/ما-حكم-من-قدمت-السعي-على-الطواف
  • Imechapishwa: 19/01/2025