Hukumu ya kuvaa nguo ya rangi nyekundu

Swali: Ni ipi hukumu ya kuvaa nguo ya rangi nyekundu tupu?

Jibu: Baadhi ya wanazuoni wameona kuwa inachukiza kuvaa nguo ya rangi nyekundu tupu isiyokuwa na mchanganyiko mwengine. Wengine hawakuchukizwa na jambo hilo kutokana na kusimuliwa kwa Hadiyth nyenginezo zinazotamka kwa kuachia kuvaa mavazi mekundu na meusi.

Swali: Ni yepi maoni sahihi?

Jibu: Allaah ndiye mjuzi zaidi. Kinachodhihirika ni kwamba inajuzu kuvaa nguo nyekundu. Hilo ndio sahihi zaidi. Hadiyth zilizopokelewa kuhusu kuvaa nguo nyekundu ni Swahiyh na zimethibiti zaidi.

Swali: Vipi ikiwa vazi hilo jekundu ni la umashuhuri?

Jibu: Haijuzu kuvaa vazi la umashuhuri; ni mamoja jekundu, kijani kibichi, jeusi wala jeupe.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23284/ما-حكم-لبس-الاحمر-الخالص
  • Imechapishwa: 20/12/2023