344 – Ameeleza[1] tena kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

المرأةُ عورةٌ، وإنّها إذا خرجتْ مِن بَيتِها استَشْرَفَها الشيطان ، وإنّها لا تكون أقربَ إلى الله منها في قَعر بيتها

“Mwanamke ni uchi. Hakika mambo yalivyo ni kwamba anapotoka nyumbani kwake basi shaytwaan humfuatishia macho[2]. Anakuwa karibu zaidi na Allaah ndani kabisa ya nyumba yake.”[3]

Ameipokea at-Twabaraaniy katika “al-Mu´jam al-Awsatw”. Wanaume wake ni wanaume wa Swahiyh.

[1] Bi maana Ibn ´Umar.

[2] Bi maana kumwangalia kwa matarajio ya kumpotosha.

[3] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/260)
  • Imechapishwa: 20/12/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy