Swali: Je, mtu ang´olewe jino la dhahabu alilokufa nalo?

Jibu: Bora waling´oe ili wanufaike nalo na waliuze.

Swali: Mavazi yake?

Jibu: Hapana. Avishwe meno mengine kama ya fedha au madini mengine. Haifai kuvaa dhahabu isipokuwa wakati wa dharurah isipowezekana kuvaa kitu kingine.

Swali: Huku si kunaingia kumkatakata viungo maiti kule kumg´oa jino lake la dhahabu?

Jibu: Hapana, sio kumkatakata viungo vyake. Ni jambo jepesi kumtoa nalo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23283/حكم-لبس-اسنان-الذهب-وهل-تقلع-من-الميت
  • Imechapishwa: 20/12/2023