Hukumu ya kuoa wanawake wasioswali

Swali: Nimepata idhini na nchi ya kuoa mwanamke ambaye anaeshi nje ya Saudi Arabia. Nimesikia Fatwa inayosema ndoa na mwanamke ambaye haswali haisihi. Je, fatwa hii ni sahihi?

Jibu: Ndio, fatwa hii ni sahihi. Kama kuna mkataba wa ndoa baina ya wanandoa wawili na mmoja wao akawa haswali, ndoa hii inazingatiwa kuwa si sahihi. Hili ni kwa sababu yule asiyeswali ni kafiri kutokana na maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Ahadi iliyopo baina yetu na wao ni swalah, hivyo mwenye kuiacha amekuru.”

“Baina ya mtu na kufuru ni mtu kuacha swalah.”

Kutokana na haya ni wajibu kuoa wanawake ambao wanaswali tu.

Check Also

Kaoa mwanamke wa Ahl-ul-Kitaab ambaye hataki kuingia katika Uislamu

Swali: Nimeoa mwanamke wa Ahl-ul-Kitaab kabla ya kuwa na msimamo, na nimepewa fatwa na baadhi …