Hukumu ya kuzini na mwanamke kisha mwanaume huyo akamuoa

Nilimuuza Ahmad kuhusu mtu ambaye anafanya uzinzi na mwanamke na kisha baada ya hapo akamuoa. Akasema:

“Inajuzu ikiwa huyo mwanamke ametubia.”

Ibn ‘Umar aliulizwa kuhusu mtu ambaye anafanya uzinzi na mwanamke na kisha baadae akamuoa. Akajibu:

“Huanza kwa uzinzi na kuishia kwa kufanya ndoa.”

Sa´iyd bin al-Musayyab aliulizwa kuhusu mtu ambaye amefanya uzinzi na mwanamke. Je, inajuzu kwake [huyo mwanaume] kumuoa? Akajibu:

“Hatujui kuwa wanaweza kutubia katika njia nzuri na kutenda kitendo kizuri isipokuwa kwa njia hii.”

  • Mhusika: Imaam Harb bin Ismaa´iyl al-Karmaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Masaa’il-ul-Imaam Ahmad wa Ishaaq bin Rahuuyah, uk. 57
  • Imechapishwa: 22/09/2020