Swali: Hadiyth isemayo:

“Mwenye kumsitiri mtu basi Allaah atamsitiri.”

Je, inafaa kwetu kumsitiri mzinifu na mwenye kunywa pombe? Jibu ikiwa “ndio” ni vipi tutakemea maovu? Je, tupuuzie tukiona maovu?

Jibu: Mambo yakifika kwa wahusika haifai kwetu kusitiri. Ama kabla ya hapo mtu anatakiwa kutazama; je, mtu huyu alikuwa ni mwenye msimamo na akatokewa na kuteleza na huenda akinasihiwa atatubu kwa Allaah (´Azza wa Jall). Mtu kama huyu lililo bora ni kumsitiri[1]. Lakini ikiwa kwamba kumsitiri atakuwa muovu zaidi na shari yake itazidi haijuzu kumsitiri. Bali ni lazima kuwafikishia watawala ili wamsimamishie adhabu ambayo ni wajibu kusimamishiwa.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/mzinzi-anayetakiwa-kusitiriwa/

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (74) http://binothaimeen.net/content/1721
  • Imechapishwa: 22/08/2020