3460- Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Ingelikuwa ni bora zaidi iwapo ungelimsitiri kwa nguo yako.”

Ameipokea Abu Daawuud, an-Nasaa’iy katika “as-Sunan al-Kubraa”, al-Haakim, al-Bayhaqiy, Ibn Abiy Shaybah, Ahmad na Ibn ´Abdil-Barr katika “at-Tamhiyd”.

Kwa ufupisho Hadiyth inatumiwa kwa watu mfano wa Maaiz ambaye ametubia juu ya uzinzi na si mazowea yake uzinzi. Mtu kama huyu anatakiwa kusitiriwa na kutomfedhehesha. Hata hivyo haitakiwi kumficha mtu ambaye amesheheni kwa uzinzi na anajulikana vyema kwa madhambi. Mtu kama huyu anatakiwa kufichukuliwa na kushtakiwa mahakamani ili asimamishiwe adhabu ya Kishari´ah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Ahaadiyth as-Swahiyhah (7/3/1636)
  • Imechapishwa: 28/07/2020