Hukumu ya kuchelewesha hajj pasina udhuru

Swali: Ni ipi hukumu ya ambaye anachelewesha kuhiji pasi na udhuru ilihali ni muweza?

Jibu: Ambaye anachelewesha kuhiji na hajahiji ile hajj ya kwanza ambayo ni faradhi na akachelewesha pasi na udhuru, basi hakika amefanya maovu na dhambi kubwa. Ni lazima kwake kutubu kwa Allaah kutokamana na jambo hilo na kuharakisha kuhiji. Allaah (Subhaanah) amesema:

وَلِلَّـهِ عَلَى النَّاسِ حِجُّ الْبَيْتِ مَنِ اسْتَطَاعَ إِلَيْهِ سَبِيلًا ۚ

”Kwa ajili ya Allaah ni wajibu kwa watu watekeleze hajj katika Nyumba hiyo kwa mwenye uwezo wa kuiendea.” (93:97)

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Uislamu umejengwa juu ya vitano; kushuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah, kusimamisha swalah, kutoa zakaah, kufunga Ramadhaan na kuhiji Nyumba.”[1]

Kuna maafikiano juu ya usahihi wake.

Vilevile maneno yake (Swala Allaahu ´alayhi wa sallam) wakati Jibriyl alipomuuliza kuhusu Uislamu. Hadiyth hiyo ameipokea Muslim katika “as-Swahiyh” yake[2].

[1] al-Bukhaariy (16) na Muslim (8)

[2] Muslim (08)

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (16/353)
  • Imechapishwa: 26/05/2022