Swali: Ni yapi maoni yako kwa mwenye kusema ´tukiafikiana kwenye msingi wa dini – yaani Tawhiyd – tupeane udhuru kwa mambo mengine yote ya dini`?

Jibu: Hapana hawasemi hivi. Wanasema ´tuwe na umoja kwa yale tunayoafikiana` na hawasemi msingi wa dini wala Tawhiyd. Wanasema ´tuwe na umoja kwa yale tunayoafikiana na tupeane udhuru kwa yale tunayotofautiana`. Husema hivi. Ama msingi wa dini na Tawhiyd hawasemi hivi kamwe. Wanasema kuwa mambo haya yanawatofautisha watu. Wanasema kuwa Tawhiyd inawatofautisha watu. Msitake Tawhiyd kutoka kwa watu au mkawaamrisha Tawhiyd na kuacha yale waliyomo kwa kuwa mambo haya yanawatofautisha watu. Hivi ndivyo wanavyosema.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (22) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1428-3-7.mp3
  • Imechapishwa: 19/08/2020