Maiti ameacha anausia azikwe na Qur-aan

Swali: Kuna kijana ameuasi akizikwa azikwe na Qur-aan. Ni ipi hukumu ya wasia huu?

Jibu: Asizikwe na Qur-aan. Usitekelezwi sampuli ya wasia kama huu. Haijuzu kuutekeleza. Haijuzu kuzika Qur-aan na maiti. Usitekelezwi kwa kuwa ni kuisaliti Qur-aan na ni Bid´ah. Hakuna kinachomnufaisha mwanaadamu isipokuwa matendo yake. Haijalishi kitu hata kama atazikwa na misahafu mia hakuna kitachomnufaisha isipokuwa matendo yake aloyafanya. Ikiwa alitenda kwa mujibu wa Qur-aan atapata malipo ya kheri na neema kutoka kwa Allaah (´Azza wa Jall) hata kama hatozikwa na Qur-aan. Ikiwa ametenda maovu hata kama atazikwa na Qur-aan haitomnufaisha kitu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (23) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1428-3-14.mp3
  • Imechapishwa: 19/08/2020